Nyimbo Mpya: Mbosso, Anjella Wang'aa Kwenye Nyimbo Tano Bora Wiki Hii
17 March 2021
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Branice Nafula
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mchipuko wa nyimbo mpya kutoka bongo unaendelea kung'aa huku wasanii wageni wakiingia kwenye orodha ya nyimbo tano bora. Hivyo, kwenye nakala hii tunaangazia nyimbo tano bora kwenye YouTube Tanzania wiki hii:
Yalah - Mbosso
‘Yalah’ ni wimbo yenye maudhui ya mapenzi. Kwenye wimbo huu, Mbosso anaeleza kuwa mtu yeyote anaweza kupata mapenzi licha ya kule anakotoka au kazi anayofanya. Video ya wimbo huu imepokelewa vizuri na ina watazamaji zaidi ya Millioni moja nukta tatu kwenye mtandao wa YouTube.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Nandy Zinazovuma Bongo
Superwoman – Tanzania Men All-stars
Wasanii wa kiume mashuhuri Tanzania waliachia wimbo huu maalum kwa ajili ya kusheherekea siku ya wanawake iliyoadhimishwa tarehe 8 mwezi huu wa Machi. Hivyo, ‘Superwoman’ ni wimbo wa kuunga na kuthamini harakati na mchango wa wanawake katika jamii. Wasanii husika walienda katika studio za wasafi FM Kuuzindua wimbo huu rasmi na kufikia sasa kanda ya kipindi hiki kina awatazamaji zaidi ya laki sita kwenye YouTube.
Kama - Anjella ft Harmonize
Wimbo huu ni wa maudhui ya mapenzi ambapo waimbaji hao wanaangazia hulka na tabia za watu wanaotaka kuwa na uhusiano nao. Anjella anamuomba Mungu ampe mtu mwenye mapenzi ya kweli na si wa kumuhadaa. Ikiwa kazi yake ya kwanza wimbo huu umefikisha watazamaji zaidi ya laki tano.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Video Mpya Kwa Jina 'Yalah'
Leo Leo - Nandy Ft Koffi Olomide
Huu ni wimbo wa Kilingala ambapo Nandy na Koffi Olomide wanatumia lugha nyingi zikiwemo Lingala, Kiingereza na Kiswahili. Wimbo huu umetayarishwa na Kimambo na unahusu mapenzi. Waimbaji wote wanatafuta umuhimu wa kumtuliza mpenzi kwa uhusiano mzuri.
Baikoko - Mbosso ft Diamond Platnumz
Huu ni wimbo mojawapo kutoka albamu ya Mbosso ya ‘Definition of Love’. Baikoko ni wimbo wa densi na una maudhui ya mapenzi ambapo waimbaji hawa wanasifia minenguo ya mpenzi wao. Kufikia sasa wimbo huu una watazamaji zaidi ya laki tano huku video yake ikitarajiwa hivi karibuni.
Leave your comment