Nyimbo Mpya: Rayvanny Awaongoza Wasanii wa Bongo Kuachia Nyimbo za Kuomboleza Magufuli

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Tanzania inapoendelea kuomboleza kifo cha Rais wa awamu ya Tano marehemu Rais John Pombe Magufuli, wasanii wa nchi hiyo wameachia nyimbo za kumkumbuka. Katika nakala hii, tunaangazia baadhi ya nyimbo hizo huku ikitarajiwa kuwa nyimbo zingine zitaachiwa hivi karibuni.

Kifo - Rayvanny

Katika wimbo huu Rayvanny anamlilia rais wake akisema ‘Kifo’ hakina huruma, kuwa kinachukua wema tu kwanini huku akiuliza nani atawafuta machozi?

https://www.youtube.com/watch?v=McqT-XpgYhQ

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso, Anjella Wang'aa Kwenye Nyimbo Tano Bora Wiki Hii

2060 - Madee Ali

Kwenye wimbo huu, Madee anamsifu Rais Magufuli kwa maendeleo aliyofanya kwa miaka mitano aliyokuwa uongozini.

https://www.instagram.com/tv/CMiNId_DGr3/?utm_source=ig_web_copy_link

Magufuli Umetuacha Imara - Peter Msechu

Mwimbaji Peter Msechu naye kaachia wimbo huu akisema Magufuli ameiacha Tanzania salama. “Raisi wetu sisi watanzania tumebaki wakiwa hatuna la kufanya ila ni ukweli usio na kipimo kuwa "Umetuacha Imara".

https://www.youtube.com/watch?v=l6WIWBKVI6o

Konde Music Artists - Asante Magufuli

Wasanii wa lebo ya Harmonize wameandaa wimbo wa kumshukuru marehemu Rais Magufuli kwa kupigania maslahi ya wanyonge nchini humo. Kwao wanasema kama nchi walimpenda rais wao ila Mungu kampenda zaidi.

Soma Pia: Nyimbo 5 za Singeli Zinazovuma Bongo Machi 2021 [Video]

https://www.youtube.com/watch?v=YgIKXLUt428

Kwingineko, wasanii wengine tajika wameonekana kukesha studio wakirekodi wimbo maalum wa kuomboleza kifo cha Rais huyo.

Wasanii hao ni kama vile Diamond Platnumz, Madee, Lavalava, Bi. Khadija Kopa, Zuchu, Christina Shusho, Gnako, Ben Pol, Mbosso, Karen, Dulla Makabila miongoni mwa wengine.

 

Leave your comment