Nyimbo 5 za Singeli Zinazovuma Bongo Machi 2021 [Video]

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Muziki wa Singeli ni mojawapo ya aina za muziki kutoka Bongo inayoendelea kukua kwa kasi.

Wasanii wa nyimbo hizi wanajikakamua kila kukicha ilikufanikisha uwezo wa muziki huo. Katika nakala hii, tunaangazia nyimbo tano za Singeli zinazovuma mwaka huu 2021:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Meja Kunta Aachia Video Mpya ‘Madanga ya Mke Wangu’Akimshirikisha D Voice

Sema Kweli – Dulla Makabila

‘Sema kweli’ ni wimbo wa michambo ambapo Dulla Makabila ameamua kusema ukweli wake kuhusu mahusiano yaliyomo miongoni mwa wasanii wa Bongo. Katika kanda hii, Makabila amefunguka namna mtangazaji maarufu Majizzo na Chibu ambaye ni Diamond hawapendani katu miongoni mwa mambo mengine ya bongo. Kufikia sasa wimbo huu una watazamaji zaidi ya laki sita kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=1YYzIUTl1wE

Madanga ya Mke wangu - Meja Kunta ft D Voice

‘Madanga ya Mke wangu’ ni wimbo kuhusu uzuri wa udangaji wa mwanamke kwenye ndoa. Kwa kifupi wawili hao wanaangazia hadithi ya mwanamume mmoja ambaye amefanya madanga ya mke wake kuwa biashara ya kujikimu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Nandy Zinazovuma Bongo

https://www.youtube.com/watch?v=NaPt97DwWzY

Nimeghairi Kufa - Dulla Makabila

‘Nimeghairi Kufa’ ni wimbo wenye ujumbe mzito unaotukumbusha kuwa maisha ni mafupi, hivyo ni muhimu kuzingatia chanzo cha furaha yako. Kwingineko anaangazia kile anachodhani hakitatendeka kwenye mazishi yake. Wimbo huu unawatazamaji zaidi ya milioni moja nukta mbili.

Pakua Nyimbo Zake Meja Kunta Bure Kwenye Mdundo

https://www.youtube.com/watch?v=OnVTBo2SpDY

Kwa Mganga - Msomali

Huu ni wimbo wa Msomali ambapo anaangazia mwanamume mmoja aliyejaribu kujitoshanisha na mganga katika kutafuta mpenzi. Kufikia sasa wimbo huu unaendelea kupata umaarufu huku ukiwa na watazamaji zaidi ya elfu sabini kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=7wapmAKmZHs

Shegua - Balaa MC

Huu ni wimbo wa kuburidika na kujipa raha. Shegua ina midundo mizur hawa kwa wale wanaopenda ngoma za kale. Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya laki nne.

https://www.youtube.com/watch?v=byqZt_9jpa0

Leave your comment