Tofauti Nne Kuu Kati ya Bongo Fleva ya Zamani na ya Kizazi Kipya

[Picha: Nairobi News]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Muziki wa Bongo Fleva umekua ukiamarika kila kukicha. Teknologia imesaidia kuimashira midundo na ata video zinazoachiwa na wasanii wa Bongo.

Katika nakala hii, tunaangazia tofauti kuu kati tya bongo fleva ya zamani na ile ya kizazi kipya:

Soma Pia: Mixes Tano Bora za Kupakua Kwenye Mdundo Wiki Hii

Uhalisi

Katika miaka ya hivi karibuni muziki wa Bongo umepata sauti ambazo wengi wanaona kama umepotoza uhalisia wa muziki wa bongo fleva. Hapo awali muziki wa bongo ulikisiwa kuwa muziki wa kitofauti kawa sababu wasanii walizingatia maudhui ya kuaminika kama vile mapenzi na machungu yake.

Mienendo (Trends)

Awali wasanii walitegemea vyombo vya habari kuafikiana na mienendo au kujua kama nyimbo zao zinafanya vizuri. Pia wasanii wengi walitegemea tamsha mbali mbali ili kupata nafasi ya kuuza muziki wao ili kujipatia kipato. Wakati huu wa teknojia umechangia usambazaji wa mziki na wasanii wa mziki wa bongo sasa wanatumia utandawazi katika kuuza mziki wao. Wengine wanapata fursa ya kuwa kwenye orodha ya nyimbo bora haswa katika mitandao ya kusambaza mziki.

Soma Pia: Pakua Mixtapes 5 Kali za Diamond Platnumz Kwenye Mdundo

Ubunifu

Wasanii wenye ushawishi mkubwa ni wasanii wa zamani, waliofanya mziki kwa sababu ya ujumbe ambao walitumia. Ubunifu wa Bongo Fleva ulikua wa kuunganisha kila kitu katika jamii kwani wasanii walionekana kama wawakilishi wa jamii. Tofauti ilioko na sasa ni kuwa wasanii sasa wanashabikia kiki, basi imeshusha ubunifu wa wasanii wengi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Nandy Zinazovuma Bongo

Ushindani kati ya wasanii

Kumekua na ushindani kati ya wasanii wa bongo flava ya sasa huku wachache wakiwa kwenye kilele cha sanaa na muziki wao. Joto hili la ushindani kati ya wasanii wa Tanzania linazidi kupanda huku mashabiki na wanahabari wakidaiwa kuchochea hilo kwa namna moja au nyingine. Hii inaleta tofauti na zamani ambapo wasanii kazi yao kubwa ilikua kutengeza mziki kwa ajili ya kukuza talanta na uonyeshaji wa rasilmali Tanzania. Wimbo kama Leka Dutigite ya Kigoma All Stars ilikua na wasanii wote kutoka Kigoma kazi iliyowafurahisha mashabiki wa Tanzania.

Leave your comment