Pakua Mixtapes 5 Kali za Diamond Platnumz Kwenye Mdundo

Jiunge Nasi Kwenye Telegram

Fani ya mziki wa Tanzania inaendelea kukua ila kukicha. Katika kuwapa heshima na hadhi wanamziki hao, wanasanturi pia wameshika dau katika kutengeza mixes moto za mziki.

Katika nakala hii, tunachambua mixtapes tano kali za Diamond Platnumz unazofaa kupakua wiki hii:

Bongo mix 2021 ya DJ BEE

Hii ni mix yenye mchanganyiko wa muziki wa  Diamond Platnumz, Marioo, Bontle Smith, Sho Madjozi ,Dully Sykes na Harmonize. Katika mix hii lengo ni kukuburudisha wewe shabiki wa wasanii hawa ukiwa kwenye pilka pilka zako za kila siku.

Best of Bong mix vol #3 Dj BEE

Hii hapa ni mchanganyiko wa nyimbo za mapenzi kutoka kwa Diamond Platnumz, Rayvanny, Rommy Jons, Harmonize ,QChilla na Masauti wa Kenya. Burudisha umpendaye kwa kupakua mix hii hapa kali ili kukoleza mapenzi yenu.

Diamond , Khaligraph, Aya Bongo Mix by DJ BEE 

Huu ni mchanganyiko wa nyimbo za upendo na za kudensi. Ubabe wa Diamond kwenye mix hii umedhihirishwa kwa wimbo wa ‘Jeje’, huku Rema wa Nigeria akijumuishwa humu pamoja na Aya Namukura wa Uganda pamoja na Khaligraph na Masauti wa Kenya. Pakua mix hii ujiburudishe vilivyo.

Jeje, Ommy Dimpoz, Nandy Mix Dj Bee

Hii hapa ni mchanyiko wa mziki kutoka kwa Diamond Platnumz, Nandy, Ommy Dimpoz ambao ni wasanii wenye ujuzi mkubwa. Mwanasanturi DJ Bee anakupa nafasi ya kufurahia mziki mzuri kutoka kwa wasanii hawa tajika.

 

Diamond Platnumz,Simi, Aslay, Rema Bongo Mix 2021 by Dj Bee

Hizi nyimbo kama vile Baila na Wakawaka mojawapo ya kazi kubwa kutoka kwa mwanamziki Diamond Platnumz. Wasanii wengine husika katika mix hii ni kama vile Simi wa Nigeria na Rema. Pakua mix hii ufurahie mziki moto.

Leave your comment