Mbosso Aeleza Alivyotafuta Majibu ya Albamu Yake Mpya ‘Definition of Love’

[Picha: Mdundo Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Jiunge Nasi Kwenye Telegram

Msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva Mbosso anatarijiwa kuachia albamu yake mpya ‘Definition of Love’, tarehe 13, mwezi huu wa Machi.

Huku mashabiki wakitarajia kuona ubabe wake katika kutafuta maana halisi ya Upendo, Mbosso ameachia kanda mbili zinazoonyesha namna alivyofanya utafiti wake.

Hivi katika maisha kila binadamu anatamani kupendwa ila si wengi wanajua maana au umuhimu wa upendo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Collabo 5 Zake Diamond Zinazovuma Bongo [Video]

Mara nyingi watu wanaamini kuwa uhusiano kati ya watu wawili ndio upendo. Hivyo Mbosso anauliza je ni nini maana ya upendo. Katika kanda hizi tunaona Mbosso akikutana na Said Mayweather mkali wa kuziba pancha ambaye ana maelezo yake ya maana ya mapenzi.

“Mapenzi ni Hisia ,Yani ni hali ya watu wawili wanapokuwa kwenye hisia moja au hisia zinazoshabiriana.” alisema Said.

Akaenda kwingine kwenye hoteli moja ya Kazagata ambapo aliwapata watu tofauti waliotoa maana ya mapenzi kwao.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Kumi Bora Tanzania Februari 2021

Salim alisema kuwa mapenzi ni kumpenda mtu kutoka Moyoni huku Baba la Baba akisema kuwa na mkewe ndio maana ya mapenzi kwake.

Mzee mazuna akatinga kwa kusema kuwa mapenzi ni uvumilivu. Haji naye akawa na jibu la kutokuwa na mpenzi ila upendo wake ni wa mpira.

Hivyo ukitazama kanda hizi unamuona Mbosso na kijitabu anapoandika kila anachoambiwa na watu hawa. Kwa kiasi hili ni dhihirisho kuwa Mbosso alitumia njia hizi za utafiti kusaidia katika uandishi wa nyimbo za albamu hii ‘Definition of Love’. Je, wewe unaamini Mapenzi ni Nini?

Leave your comment