Q Chief Aomba Radhi kwa Kuwatusi Diamond na Usimamizi Wake

[Picha: Q Chief Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Jiunge na Channel ya Mdundo Telegram

Msanii wa mziki kutoka Tanzania Abubakar Katwila almaarufu Q Chief amewaomba msamaha Diamond Platnumz, meneja wake Sallam Sharaf, mashabiki na washikadau wa muziki nchini Tanzania kwa kumtusi Diamond Platnumz.

Qchief alisema hayo katika mazungumzo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Dulla Makabila Aachia Video Mpya ‘Sema Kweli’

Hii ni baada ya video kusambaa mtandaoni ambapo Q Chief aliwapasha na kuwatusi Diamond na meneja wake.

Katika video hiyo, Q Chief pia alisikika akitoa tuhuma za kutumika kwa picha yake kwenye bango linaloonyesha orodha ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha la Wasafi ‘Tumewasha’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam Januari 31, 2021.

Download Q Chief Music for Free on Mdundo

Q Chief alilalamika kuwa licha ya picha yake kuonekana hakuwa na fahamu wa uhusika wake kwenye tamasha hilo na wala hakualikwa. Akizungumza na waandishi wa habari Februari 27, 2021, msanii huyo amesema alichukizwa na jambo hilo na hasira ndio zilimfanya kutoa lugha chafu mtandaoni.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video Mpya ‘Leo Leo’ Akimshirikisha Koffi Olomide

“Kwanza kabisa ni kuomba radhi kwa clip ambayo imekua ikitembea ambayo ina lugha ama inakiuka maadili ya Kitanzania, kama kaka kama legend, kama inspiration to this generation…Nilikua na hasira mi mwandamu ambaye sijatimia wa hiyo pengine nilitoka nje ya msingi…” alisema Q Chief.

Hata hivyo, msanii huyo alisisitiza kuwa anaomba radhi tu kwa matamshi yake ila mengine kuhusu show ya ‘Tumewasha’ bado anafuatilia kisheria.

Leave your comment