Nyimbo Mpya: Dulla Makabila Aachia Video Mpya ‘Sema Kweli’

[Picha: Dulla Makabila Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Tumia Rafiki kwenye WhatsApp

Mfalme wa Singeli Dulla Makabila ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Sema Kweli’.

‘Sema kweli’ ni wimbo wa michambo ambapo Dulla Makabila ameamua kusema ukweli wake kuhusu mahusiano yaliyomo miongoni mwa wasanii wa Bongo.

Soma Pia: Wimbo ‘Nimeghairi Kufa’ wake Dulla Makabila Wafikisha Watazamaji Milioni Moja

Katika kanda hii, Makabila amefunguka namna mtangazaji maarufu Majizzo na Chibu ambaye ni Diamond hawapendani katu.

Akiendelea anasema jinsi mwimbaji Ruby bado anampenda Kusah na anapata tabu, huku akisema Kiba kajua kuimba, akiongezea Uchebe vile ni mshamba.

Download Dulla Makabila Music For Free on Mdundo

Kwenye fungu lifuatalo, Makabila anamsuta Babalevo akisema anastahili taji kwa uchawi, na kuongeza kuwa ni kweli Nandy kapenda ila tu Nenga si muoaji.

Anamalizia kwa kusema kuwa hasira ya Konde ni Sarah ila Paula akawa sababu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video Mpya ‘Leo Leo’ Akimshirikisha Koffi Olomide

Wimbo huu uliojaa michambo na kiki za Tanzania ni wimbo ulio na ubunifu mkubwa. ‘Sema Kweli’ imepokelewa kwa ukubwa sana huku wanamziki wengine wakipata kufurahishwa na utunzi wa Dulla.

Maandalizi ya wimbo huu ilifanywa na Director Majagi. Video ya wimbo huu inaendela kupata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube ikiwa na watazamaji zaidi ya elfu ishirini na saba.

https://www.youtube.com/watch?v=1YYzIUTl1wE

Leave your comment