Wimbo ‘Nimeghairi Kufa’ wake Dulla Makabila Wafikisha Watazamaji Milioni Moja
28 January 2021
[Anwani ya Picha: DUulla Makabila Instagram]
Mwandishi: Branice Nafula
Msanii tajika wa mziki aina ya Singeli Dulla Makabila ni mwenye furaha baada ya wimbo wake “Nimeghairi Kufa” kufikisha watazamaji milioni moja kwenye mtandao wa YouTube. K
‘Nimeghairi Kufa’ ni wimbo wenye ujumbe mzito unaotukumbusha kuwa maisha ni mafupi, hivyo ni muhimu kuzingatia chanzo cha furaha yako.
Read Also: Dulla Makabila Drops New Singeli Hit ‘Nimeghairi Kufa’ [Video]
Kupitia mtandao wa Instagram, Makabila amewashukuru mashabiki kwa kutazama kazi yake na kumtia motisha kuendelea kutunga na kuachia wimbo zingine.
Hii hapa ujumbe wake Dulla Makabila:
Kiukweli Nina Furaha isiyoelezeka Muziki Wa Singeli Nauona Mbali Sana Ni Kiasi Gani Mungu Ametuonesha Mwanga Na Kutupa Heshima Maana Tulipoutoa Mpaka Ulipofika Sio Kitu Kidogo Leo #NimeghairiKufa imepata Views 1m Ndani Ya Mwezi Mmoja Kitu Ambacho Hakijawai Kutokea Tangu Mziki Wa Singeli Uanze Naomba Nieke Sawa hapa ili Wasanii Wenzangu Wa Singeli Wasije Kujiskia Vibaya Sina Maana Kuwa Hakuna Wimbo Wa Singeli Ulowai Kutimiza Milioni Zipo Ila Sio Ndani Ya Mwezi Mmoja Asante Mungu.
Download Dulla Makabila Music For Free on Mdundo
Hii Ni Moja Ya Hatua Kubwa Sana Katika Mziki Wangu Sina Budi Kuwashukuru Mashabiki Zangu Na Media Zinazonisapoti Na Ata Zisizonisapoti Na Pia Niishukuru Team Yangu Nzima Ya #MiRangiEmpire Tulioshilikiana Kukamilisha Video Yetu Asanteni Sana Nawapenda Sana Tanzania nzima yupo king of Singeli Mmoja Tu Na Akifa Taifa Limepata Hasara.Maneno bila vitendo ndo ujinga naoukatazaga.
Read Also:Roma Retires from Music, Drops Last Song Dubbed ‘Diaspora’ Featuring Lady Jaydee [Video]
Leave your comment