Kayumba: Msani Tajika Anayezidi Kuimarika Kila Uchao

[Picha: Kayumba Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Kayumba ni miongoni mwa wasanii wanaochipuka kwa kasi kwenye anga ya muziki wa Tanzania.

Katika tasnia iliyojaa zaidi, Kayumba kama staa mwingine wa muziki huweka mtiririko thabiti katika matoleo yake. Kayumba alipata umaarufu baada ya kushinda tuzo na shilingi milioni hamsini kwenye Bongo star search mwaka 2015.

Download Kayumba Music for Free on Mdundo

Hapo alipata nafasi ya kuendeleza talanta yake kwa uthamini wa Bi Rita Paulsen aliyemsaidia na ada ya kulipia kazi yake ya kwanza kabisa ya wimbo ‘Katoto’.

Wakati huo huo Kayumba alikua katika lebo ya Mkubwa na Wanawe ambayo ilikua chini ya usimamizi wa Mkubwa Fella na Babu Tale. Tangia mwaka 2016, Kayumba ameachia kazi zake nzuri zikiwemo ushirikiano wake na Enock Bella kwa wimbo ‘Kipepeo’, Mama, Chunga, Talalila, Nimezidiwa akimshirikisha Isha Mashauzi na nyinginezo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Kayumba Aachia Video Mpya ya Wimbo Wake ‘Bomba’

Huku akijaribu kuwa miongoni mwa wasanii tajika kutoka Bongo, Kayumba bado anatangamana na changamoto za wasanii kutoka lebo kubwa Tanzania na wenye umaarufu mkubwa zaidi. Hivyo Kayumba hajapata fursa ile tunayoweza kusema ni ya usawa kabisa.

Iwapo angepata nafasi kama ile ya wanamziki wengine au uthamini wa kuwa ndani ya lebo kubwa basi naamini Kayumba ni mwanamziki wa kufananishwa na magwiji kama vile Diamond Platnumz, Mbosso na hata Alikiba.

Kazi yake mpya ‘Bomba’ ni dhihirisho wa ujuzi wa Kayumba katika fani ya mziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Album Mpya 'Sound from Afrika'

‘Bomba’ ni wimbo uliowafanya wasanii wengine kama Maua Sama na Roma kuumpa staa huyo heko kwa kazi ya nzuri na motisha ya kufanya mziki zaidi.

Kwingineko msanii kutoka Kenya Nadia Mukami ameonyesha hamu ya kufanya remix ya wimbo huo Bomba na Kayumba.

https://www.youtube.com/watch?v=ngHoTiBSBzo

Leave your comment