Nyimbo Mpya: Kayumba Aachia Video Mpya ya Wimbo Wake ‘Bomba’

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Branice Nafula

Mwandishi na msanii wa nyimbo za mapenzi kutoka Tanzania Kayumba ameachia kanda ya wimbo wake mpya ‘Bomba’.

‘Bomba’ ni toleo jipya la maudhui ya upendo ambapo Kayumba anaelezea ni kwa nini anampenda mrembo wake.

‘Bomba’ ni neno la Kiswahili linalomanisha sawa yaani yuko sawa kabisa. Katika mistari ya wimbo huu tunaona ubunifu wa ushairi wa Kayumba anapomsifia mpenzi wake. “Ah jicho kokodo ukinikodolea,Huo mkonyezo mwenzake najilegea, Chuzi la sotojo limenikolea,Mi mbwa mbele ya chatu, Hata linasogelea,Tupendane tuwe kati ya makumbusho…”

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Album 4 Zinazofanya Vizuri Bongo Mwaka wa 2021

Kanda ya wimbo huu imetengezwa kwa ujuzi mkubwa huku mitambo ya mziki iliyotumika hapa pia ikiwa ya hali ya juu.

Waandaji wa kazi hii ni pamoja na director Majagi na Producer Mr. T Touch.

‘Bomba’ ni kazi yake ya kwanza mwaka huu, huku akiendelea kudhihirisha ubabe wake katika fani ya mziki wa Bongo.

Download Kayumba Music for Free on Mdundo

Kayumba amekua kwenye mziki kwa zaidi ya miaka minne sasa baada ya kushiriki katika shindano la Bongo star search mwaka wa 2015.

Hivyo, yeye ni mojawapo ya wasanii wa kizazi kipya wanaojaribu kujijengea riziki kupitia sanaa.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Album Mpya 'Sound from Afrika'

Video hii imepokelewa vizuri na mashabiki na kufikia sasa ni ngoma iliyo na watazamaji zaidi ya elfu kumi na mbili kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=ngHoTiBSBzo&ab_channel=KAYUMBAOG

Leave your comment