Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Mpya Zinazotamba Bongo Wiki Hii

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Tumia Rafiki Kwenye WhatsApp

Wiki hii kutoka Bongo wasanii tajika wameweza kuachia mziki mpya hususan kwa ajili ya siku ya wapendanao. Katika nakala hii, tunaangazia nyimbo tano zilizovuma wiki hii:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Album 4 Zinazofanya Vizuri Bongo Mwaka wa 2021

Leo Leo - Nandy ft Koffi Olomide

Huu ni ushirikiano wa Nandy na msanii mkongwe wa mziki wa Lingala Koffi Olomide. Wimbo huu una audhui ya mapenzi . Ni wimbo unaoafikiana ana maudhui ya mwezi huu wa mapenzi. Nandy sasa ni msanii wa pili kutoka Tanzania kumshirikisha Koffi kwenye kazi yake baada ya Diamond Platnumz.

https://www.youtube.com/watch?v=vbJBI9UxSmk

Mapepe - Juma Jux

Hili ni toleo jipya kutoka wa mfalme wa nyimbo za mapenzi Juma Jux. Katika wimbo huu, Juma anasisitiza kuwa mapenzi hayataki ‘mapepe’, ila utulivu na uaminifu. Hivyo Juma anamkashifu mwanaume mmoja amabaye kazi yake ni kuruka kutoka uhusiano mmoja hadi mwingine bila ya kuthamini hisia za mpenzi wake.

https://www.youtube.com/watch?v=G0qRQhNRLcI

Sifa – Rostam ft Ben Pol

Huu ni wimbo wa mapenzi ambapo Rostam Wanmsifia dada mmoja ambaye wanampenda. Kwa kifupi ni mwanaumume anayejaribu kumteka msichana mmoja awe mpenzi wake. Ben Pol kwa upande wake hakukosea na sauti yake nzuri katika wimbo huu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Album Mpya 'Sound from Afrika'

https://www.youtube.com/watch?v=rtDHrUfP15k

Mbio – Alikiba

Huu ni mojawapo wa nyimbo zinazotarajiwa kutoka kwa albamu yake mpya hivi karibuni. ‘Mbio’ ni wimbo wa mapenzi na Alikiba anaangazia jinsi anavyompenda mwenzake na anashangaa ni mbona anahisi ni kama analazimisha mapenzi. Hivyo moyo wake unamwenda mbio na hayawezi tena mapenzi kama yale.

https://www.youtube.com/watch?v=b342dvCdlGQ

Kiuno - Rayvanny

Ni wimbo kutoka albamu ya Rayvanny ya “Sound From Afrika”. Rayvanny anaangazia namna kiuno cha mpenzi wake kinapagawisha anavyokata. Wimbo huu unaendelea kupata umaarufu zaidi.

https://www.youtube.com/watch?v=r573wpRMtaA

Leave your comment