Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Zinazotamba Bongo

[Anwani ya picha:The Citizen]

Mwandishi: Branice Nafula

Share on WhatsApp

Wanamziki kutoka Bongo wanaendelea kuonyesha ushupavu wao katika uandishi wa nyimbo. Kila kukicha wanamziki hao wanaachia nyimbo mpya ili kufikia matakwa ya mashabiki zao.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Album Mpya 'Sound from Afrika'

Katika nakala hii, tunaangazia nyimbo tano bora wiki hii kutoka bongo:

Lala – Rayvanny ft Jux

Huu ni wimbo ulio kwenye albamu ya Rayvanny na umepata umaarufi zaidi kwa sababu ya maudhui yake. Katika wimbo huu, Rayvanny na Jux wanazungumzia mapenzi yao ya awali. Wawili hao wameonyesha ubabe kupitia sauti zao.

https://www.youtube.com/watch?v=kSZxCkxUQzo

 

Sukari - Zuchu

Huu ni wimbo wake Zuchu ambao bado unashikilia nambari moja kwenye video bora Tanzania kwenye mtandao wa YouTube. Kufikia sasa wimbo huu wa mapenzi una zaidi ya watazamaji milioni tatu.

https://www.youtube.com/watch?v=CCmItvVgn6Q

Ibraah - Nimpende

‘Nimpende’ ni wimbo unaoangazia jinsi upendo unapaswa kuonekana. Wimbo huu ulitengenezwa na Wambaga na unafanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube. Ni moja ya “Karata Tatu” za Ibraah kutoka Konde Music Worldwide.

Soma Pia: Zuchu Elated after Featuring on BBC’s Top 10 African Musicians to Watch

https://www.youtube.com/watch?v=qbEA5O26mEg

Wivu –Mausama ft Aslay

‘Wivu’ ni wimbo unaongazia changamoto zilizoko kati ya wapenzi wawili na namna wao wenyewe wanajaribu kupigania penzi lao.

Zuena - Rayvanny ft Mbosso, Weasel

Hii ni mojawapo ya nyimbo kutoka kwenye album yake Rayvanny “Sound From Africa”. Zuena ni wimbo ulioingia kwenye trends kwa sababau ya ubabe wa Rayvanny, Mbosso na Weasel wa Uganda. Wimbo huu ulifanywa hapo awali na marehemu Radio na Weasel kwa lugha ya Kiganda. Hivo remix hii inaleta ukumbusho wa msanii huyo aliyekuwa maarufu Uganda na Bara nzima la Africa.

https://www.youtube.com/watch?v=YA0mVuRvl6E

Leave your comment