Zuchu Aahidi Kutamba Dunia Nzima Mwaka wa 2021
21 January 2021
[Photo Credit: Zuchu Instagram]
By Branice Nafula
Msanii maarugu kutoka Tanzania Zuchu ametangaza kuwa mwaka huu wa 2021 ni mwaka wake wa kutamba na kung’aa dunia mzima.
Akizungumza kwenye mahojiano katika kipindi cha Mgahawa kwenye radio ya Wasafi, Zuchu alisema kuwa mwaka wa 2020 ulikua mwaka wake wa kutambulishwa kwa mashabiki, lakini mwaka huu, ako tayari kutamba.
Soma Pia: Nyimbo 10 Bora Zilizotamba Bongo Mwaka wa 2020 [Video]
"Mwaka uliopita ulikuwa mwaka wa kutambulishwa, lakini mwaka huu ni mwaka wa kazi tu, nataka nifanye kazi kiasi kwamba nikifika sehemu sihitaji nitambulishwe tena kama zuchu wa Tanzania, nataka kutambulishwa kama Zuchu msanii mkubwa Duniani," alisema kwa ufupi.
Kwingineko, Zuchu aliangazia namna bosi wake Diamond Platnumz alimwambia kuwa kuna wakati itabidi ajiangazie kama msanii kivyake.
Hivyo Zuchu anaonelea kuwa ni wakati wake kudhihirisha ubabe wake katika fani ya mziki.
Read Also: Zuchu Elated after Featuring on BBC’s Top 10 African Musicians to Watch
Wiki hii, Zuchu ameachia wimbo wake wa kwanza mwaka huu kwa jina ‘Sukari’.
‘Sukari’ ni wimbo wa mapenzi ambapo Zuchu anaelezea jinsi mapenzi ni tmau kam ‘Sukari’. Wimbo huu umeandaliwa vyema na una vigezo vyote zinazohitaji ili wimbo itambe.
Wimbo huu umepokelewa kwa ukubwa sana huku video yake ikitarajiwa hivi karibuni. Kwingineko, Zuchu ametangaza ujio wa flamu ndogo itakayo angazia maisha yake kama msanii, tangu alipojiunga na WCB.
Zuchu ametangaza kuwa filamu hiyo inatarajiwa mwezi wa Aprili.
Leave your comment