Nyimbo 10 Bora Zilizotamba Bongo Mwaka wa 2020 [Video]
14 December 2020
[Anwani ya Picha: Diamond Instagram]
Mwandishi: Branice Nafula
Mwaka huu wa 2020 umekuwa na changamato mingi kwa wasanii kote duniani baada ya janga la corona kuleta vizuizi na kusimamishwa kwa tamasha mingi duniani.
Licha ya changamoto hizi, wasanii wa Bongo Flava walijitahidi na kuendelea kuachaia nyimbo moto moto. Nakala hiii inaangazia nyimbo kumi bora zilizoachiwa mwaka wa 2020:
Waah - Diamond Platnumz na Kofi Olomide
Waah ndio wimbo wenye rekodi kubwa mwaka huu wa 2020. Kupitia wimbo huo, tuliona ubabe wa vizazi viwili tofauti ambao ni Diamond Platnumz na Koffi Olomide.
Download Diamond Music for Free on Mdundo
Jeje - Diamond Platnumz
‘Jeje’ ilifungua mwaka wa Diamond kwa dhoruba. Ilianzisha ngoma ya 'Jeje' iliyoenea barani kote. Kwa mara nyingine, Diamond alionyesha ubunifu wake katika uigizaji na utunzi wa nyimbo.
Read Also: 5 Diamond’s Record-breaking Collabos [Videos]
Dodo - Alikiba
Alikiba alianzisha 2020 na wimbo ‘Dodo’ ambapo alimshirikisha mwanabiashara na mwanamitindo Hamissa Mobetto. Kupitia wimbo huu, umahiri wa sauti ya Alikiba ulijitokeza na ushairi wake kudhihirika.
Te Amo - Rayvanny na Maricoa
Wimbo wa ‘Te Amo’ ulikuwa wimbo wa kuongoza kutoka kwa 'Flowers' EP ya Rayvanny. Mandhari ya mapenzi katika wimbo huu ulifanya wengi wakaamini kuwa mapenzi ya dhati si ndoto tu.
Bedroom - Harmonize
Bedroom ilikuwa mojawapo ya wimbo kwenye albamu ya 'Afro East'. Harmonize alionyesha ulimwengu kuwa ana uwezo wa kubadili kutoka Kiswahili hadi Kiingereza na kufanya vibao.
Kaka Tuchati - Rostam
Wimbo huu wa Hip-hop uliinua ubunifu kwa kiwango kingine. Video ambayo ina mazungumzo ya simu ya video haikutumia kamera au vifaa vya gharama kubwa. Katika wimbo huu, Roma na Stamina walihamisha wafuasi wai kuhusu janga la corona na jinsi ya kuiepuka.
I Like it- Darassa ft Sho Madjozi
Baada ya kupumzika na kutoachia muziki kwa muda, Darassa alirudi tena na wimbo huu wa mapenzi wa Hip-hop. Collabo hiyo ilisimama kwa kuwa Darassa na Madjozi wangeweza kupiga Kiswahili. Abba alitengeneza beat iliyochanganya sauti ya Bongo na Afrika Kusini.
Kwaru - Zuchu
Kwaru ni mojawapo ya nyimbo kutoka kwenye EP 'I am Zuchu', wimbo huu uliwapa mashabiki mtazamo wa nini cha kutarajia kutoka Zuchu . Zuchu alituonyesha jinsi ya kuchanganya asili ya Taarab na mziki wa kizazi kipya cha bongo flava.
Acha Lizame - Nandy na Harmonize
Tangia wasanii Nandy and Harmonize kutangaza ujio wa wimbo huu, ilikuwa dhahiri kuwa “Acha Lizame” ungepata umaarufu mkubwa. Wawili hao waliunganisha uwezo wao wa uandishi wa wimbo kutupatia ngoma hii.
Unaniweza - Jux
‘Unaniweza’ ni wimbo ulionoga sana mwaka huu kutoka kwa mfalme wa mziki wa bongo fani ya RnB. Kilichojitokeza katika wimbo huu ni msimamo wa Jux kutoa maneno ya hali ya juu ya mapenzi ambayo yanavutia hadhira yoyote.
Nyimbo zingine bora zaidi kutoka 2020 ambazo haziko kwenye orodha ni pamoja na; Gwiji ya Maua Sama na Mwana FA, Zuchu na Diamond Cheche, Ushamba ya Harmonize miongoni mwa wengine.
Leave your comment