Meja Kunta Aachia Video Mpya ‘Chura Superstar’

[Photo Credit:Meja Kunta Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Msanii tajika wa mziki aina ya Singeli Meja Kunta ameachia wimbo mpya kwa jina “Chura Superstar.”

Wimbo huu unaangazia hulka za wanaume kutafta wapenzi kiholelela huku akijisifia kudanga na na kunywa kwa deni.

“….Ooh jamani dada danga usiombe chupa mi ndio chura super star, malaya wenzako wanajua nishadanga kila baa….” hii ni baadhi ya mistari ya wimbo huu.

Read Also: Meja Kunta Biography, Music Career, Awards, Relationships, and Net Worth

Kwa kifupi ni wimbo unaowachokora watu wenye hulka za kujipendekeza kwa watu ila hawana chochote cha thamani ila wanavizia vya wenyewe.

Meja Kunta anaendelea kupata umaarufu kila kukicha haswa katika fani ya Singeli ambayo pia inaendelea kukua kwa kasi.

Download Meja Kunta Music for Free on Mdundo

Ukitazama wimbo huu kwa umakini, utagundua kua Mejja Kunta amekoma zaidi katika sanaa ya utunzi kuliko jinsi alivyokua hapo awali.

Sasa hivi Sigeli inapewa kipaumbele hata katika maandalizi. Kwenye video hii ubunifu wa wasakataji densi pia ni wa kuvutia.

Hivi majuzi, Meja Kunta alishirikishwa kwa wimbo wake Karen uitwao “Sina” ambao unaendelea kufanya vizuri mtandaoni YouTube.

Read Also: Singeli 5 Moto Zinazovuma Bongo Mwaka Huu

Wimbo huu umefanyiwa maandalizi na Makers Gang. Kufikia sasa ‘Chura Superstar’ ni miongone mwa wimbo amazo zinapata umaarufu kwa kasi haswa kwenye mitandao ya mziki.

Kwenye YouTube wimbo huu unawatazamaji zaidi ya elfu themanini na nane.

https://www.youtube.com/watch?v=sdwSLp9h7Dk&feature=youtu.be

Leave your comment