Nandy Amshirikisha Alikiba Kwenye Wimbo Mpya ‘Nibakishie’

[Photo Credit:Nyimbo Mpya]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Msanii maarufu kutoka Tanzania Nandy ameachia wimbo wake mpya iitwayo “Nibakishie”. Huu ni wimbo wa mapenzi kati ya wapendanao wawili wanaoelezea wanavyopendana.

Nandy ameshirikisha mkurungenzi mkuu wa Kings records Alikiba ambaye kwa upande wake amedhihirisha ubabe wake Mistari ya wimbo huu wa “Nibakishie” ni ushairi mzuri na mdundo wake pia ni ule wa RnB fani ambayo ni umahiri wa Nandy.

Soma Pia: Nandy Speaks on Forming Music Group with Billnass

Nandy anaanza wimbo huu kwa kueleza kwa nini yeye anampenda mpenzi wake kila kukicha na namna anavyompagawisha.

Download Nandy Music for Free on Mdundo

“…Yaani, nikikutazama, naiona dunia yangu peke yangu tu, jua linapozama, giza likiingia natamani nikuine tu, ooh baby ukisakata rhumba, sijalewa nayumba” hii ni baadhi ya mistari ya wimbo huu.

Ushirikiano huu kati ya wawili hawa umekuja wakati ambapo mashabiki wamekua wakiulizia collabo kati ya Nandy na Kiba kwa muda mrefu.

Ukisikiliza wimbo huu utagundua kuwa sauti za wawili hao zinamshikamano mzuri. Alikiba anapoingia na mistari yake anakupa hisia na kumbukumbu za mapenzi ya dhati.

Hii ndio ngoma ya kwanza katiya wasanii hao wawili. Kwa sasa, wimbo huo bado haujachiliwa rasmi kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: NEW VIDEO: Nandy Drops ‘Do Me’ Featuring Billnass

Yeyote anayedai kuskiza wimbo huu ni sharti ailipe kwenye mitandao ya kuachia muziki.

Kwenye mitandao ya kijamii, mashabiki wao wamepokea wimbo huu vizuri na kuwasifi wasanii hao kwa ushiriakiano mwema.

Leave your comment