Rayvanny Asherekea Wimbo wake ‘Tetema’ Kufikisha Watazamaji Milioni Tisini

[Anwani ya Picha: Kurasa ya Instagram ya Rayvanny]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Msanii kutoka Lebo ya wasafi Rayvanny ni mwenye furaha baada ya wimbo wake wa "Tetema" kufikisha watazamaji millioni Tisini kwenye mitandao yote ya mziki.

Hii ni jumla ya Youtube, Spotify, AppleMusic, Boomplay na Audiomack.

Hii imedhihirishwa ambapo mwanamziki huyo aliweka picha ya kuonyesha nambari hiyo kwenye akaunti yake ya instagram.

Wimbo huu wa "Tetema" uliachiwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2019 ambapo Rayvanny alimshirikisha mkurugenzi mkuu wa wasafi Diamond Platnumz.

Diamond Ajumuishwa Miongoni Mwa Wasanii Wenye Umaarufu Mkubwa Afrika

Huu ni wimbo ulio na umaaraufu hadi sasa mwaka mmoja na nusu baadae.

“Tetema” ni wimbo wa furaha unaongazia faraja na starehe za wapenzi wawili. Hii ni mwanaume anamwagiza mwenzake ajishaue kimapenzi na namna anavyompagawisha.

Download Diamond Music for Free on Mdundo

Huu ni mojawapo wa nyimbo zilizozua gumzo mitandaoni kwa kuwa na mdundo wa kipekee na kuwafurahisha mashabiki kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika.

Kwenye mtandao wa YouTube wimbo huu umefikisha watazamaji million hamsini. “Tetema” sasa ndio wimbo wa kwanza wa Rayvanny kuwa na nambari hizo kubwa huku Diamond Platnumz akiongoza na wimbo wake wa “Yope Remix” ulio na watazamaji zaidi ya million mia moja ishirini na mbili.

Zuchu, Rayvanny Set to Drop New Banger

Wasanii kutoka lebo ya wasafui wanaendelea kupata umaarufu zaidi kila uchao kwa sababu ya kuachia nyimbo nzuri. Hili linachangiwa na bidii wanayozidi kuonyesha katika fani hii ya mziki wa bongo. Kwa sasa Rayvanny anatarajiwa kuachia wimbo mpya ambapo atashirikiana na Zuchu.

Leave your comment