Diamond Ajumuishwa Miongoni Mwa Wasanii Wenye Umaarufu Mkubwa Afrika

[Anwani ya Picha: Kurasa za Instagram za wasanii husika]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Msani tajika kutoka lebo ya Wasafi Diamond Platnumz ni mojawapo wa wasanii wenye wafuasi wengi kwenye mtandao wa instagram barani Afrika.

Kufikia sasa, Diamond pekee ndiye msani kutoka Tanzania ambaye ana wafuasi millioni kumi na moja kwenye mtandao huo.

Download Diamond Music for Free on Mdundo

Barani afrika sehemu ya Kusini mwa Jangwa la Sahara, yeye ndio wa tano miongoni mwa wasanii wenye umaarafu sana kwenye Instagram.

Wasanii wengine wenye umaarufu mkubwa ni wale kutoka Nigeria wakiwemo; Davido ambaye anawafuasi zaidi ya Millioni kumi na nane, akifuatiwa na Yemi Alade ambaye ana wafuasi Millioni kumi na mbili nukta tatu(12.3), naye Tiwa Savage akiwa na wafuasi Milioni Kumi na Moja nukta tisa(11.9), WizKid ni wan ne na wafuasi millioni kumi na moja nukta nne na hatimaye Diamond Platnumz akiwa na wafuasi milioni Kumi na moja.

Platnumz ni msanii aliye na uwezo mkubwa sana ambao aneandelea kuudhihirisha kila kukicha katika sanaa yake ya mziki.

Hivi maajuzi marafiki na mashabiki walishangazwa na uwezo wake Diamond alipokuwa nchini Malawi kwa tamasha la Sand Music festival. Ukitazama video zinazotamba mitandaoni mashabiki wa Malawi walikua wanaimba nyimbo zote za Diamond haswa za Kiswahili; lugha ambayo wananchi wa Malawi hawaitumii.

Hii ilikuwa dhihirisho kuwa mziki wa Diamond unatamba kote ulimwenguni na kuendelea kukuza umaarufu wake.

Leave your comment