TANZANIA: Watu wengi wananikosea - Jux

 

 

 

Msanii Juma Jux amefunguka na kusema kuwa katika maisha ya kila siku jamaa zake wa karibu ndiyo wamekuwa wakimkosea kiasi cha yeye kuvunja nao urafiki kabisa kwa kuwa wamekuwa wakimkatisha tamaa.

Jux alisema hayo kupitia kipindi cha 'Ngaz kwa Ngaz' na kudai kuwa licha ya kuvunja ushikaji na marafiki zake hao lakini yeye alishawasamehe ingawa hawezi kuwataja kwa majina watu hao.

"Unajua kuna watu wengi wananikosea hasa washikaji zangu ila siwezi kuwataja tu ila wananikosea mpaka kufikia hatua ya kuvunja urafiki nao lakini hasa ni wana ujue, katika familia watu wangu wa karibu ambao mpaka saizi niko nao sidhani kama kuna mtu alishawahi kunikosea nikashindwa kumsamehe" alisema Jux

Mbali na hilo Jux alidai kuwa wasanii kwenda kufanya video Afrika Kusini inachangiwa sana na urahisi wa kupata vitu nchini humo kama magari mbalimbali, nyumba pamoja na 'Location' nzuri kwani wakihitaji vitu hivyo kwa Tanzania "kidogo kuna ugumu katika kuvipata, hivyo wengi wanakimbilia kule kutokana na urahisi wa kupata vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kutumika kwenye video zao". Amesema Jux

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Other news