TANZANIA: Playlist yangu imejaa nyimbo za Trey Songz – Jux

 

 

 

Jux hana sababu ya kununa au kuwa na ‘wivu’ kutokana na ukaribu wa hivi karibuni kati ya mchumba wake Vanessa Mdee na staa wa Marekani, Trey Songz.

Ni kwasababu muimbaji huyo anadai playlist yake kwenye simu imetawaliwa na mkali huyo wa kuimba nyimbo za kusakia watoto kitandani.

“Nasikiliza wasanii wengi lakini playlist yangu kwenye simu msanii ambaye nyimbo zake ni nyingi ni Trey Songz,” Jux alisema kwenye kipindi cha Salama Jabir, Ngaz Kwa Ngaz.

Ni rahisi kuona hata muonekano wa muimbaji huyo mara nyingi kutaka kufanana na Trey, na hiyo inamaanisha kuwa anamuinspire kwa mengi. Jux pia amejichora tattoo kifuani inayofanana na ile ya Trey.

 

 

Kauli ya Jux inakuja katika kipindi ambacho Vanessa na Trey walikuwa karibu zaidi wakati wa kurekodi kipindi cha Coke Studio Africa na kusababisha minong’ono kuwa huenda walifanya zaidi ya kile kilichowapeleka huko.

 

 

Vee amekanusha kufanya lolote na kudai kuwa yeye na Jux wako vizuri. Jumatano hii kupitia Snapchat, Vee alipost picha hiyo chini kuashiria kuwa hali ni shwari paradiso.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Other news