TANZANIA: Wimbo wa “Roho” umeniongezea mashabiki wagumu – Christian Bella

 

 

 

Christian Bella amesema kuwa wimbo ‘Roho’ alioshirikishwa na Fid Q, umemuongezea mashabiki wengi wa muziki wa hip hop na wagumu.

Muimbaji huyo amekiri hilo wakati akiongea kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha EATV kinachoendeshwa na Salama Jabir.

“Leo kwenye Instagram natagiwa kila siku,” alisema Bella. “Watu wa hip hop wagumu hawapendagi hata tunaoimba utadhani kuna beef au nini. Yaani utasikia ‘mzee umeuaa’ wale wagumuwagumu wale, hawatakagi watu wa kuimba,” aliongeza.

Kwa upande wa Fid naye alidai kuwa Roho imemsogeza zaidi kwa mashabiki wa kike.

“Kwa ufupi tumesaidiana sababu hata DM yangu imejaa warembo siku hizi wanakuja kuniuliza ‘naomba lyrics au nini’ yaani DM yangu imekuwa lovely kidogo,” alisema Fid.

 

Unaweza kuitazama video hii hapa:

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment