TANZANIA: Billnas amesema yupo kwenye mazungumzo ya kuhamia katika label kubwa nchini

 

 

 

Msanii wa muziki wa Hip Hop anayefanya vizuri na wimbo ‘Chafu Pozi’ Billnas amesema yupo kwenye mazungumzo ya kuhamia katika label kubwa ya muziki hapa nchini hivi karibuni.

Rapper huyo ambaye kwa sasa yupo chini ya label yake ya ‘LFLG’, ameiambia Bongo5 kuwa kuna label nyingi zinamtaka kufanya naye kazi.

“Kusema kweli kuna mambo makubwa yanakuja, huwenda kazi yangu mpya ikaja nikiwa ndani ya label mpya,” alisema Billnas. Kuna label nyingi zimekuja na bado nipo kwenye mazungumzo, nadhani muda ukifika mtasikia tu,”

Billnas alianza kufanya vizuri na wimbo ‘Ligi Ndogo’ akiwa Rada Entertainment lakini baadae alihama katika label hiyo na kuanzisha label ya ‘LFLG’.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment