TANZANIA: Christian Bella asema sababu zinazomfanya azidi kufanya vizuri katika show zake

 

 

 

Mkali wa masauti Christian Bella amesema kigezo pekee cha kuwa na hit song hakiwezi kumfanya msanii afanye vizuri katika show zake

Akiongea na Bongo5 wiki hii Christian Bella amesema msanii kabla haujafanya show lazima utambue mashabiki wako huwa wanapenda kitu gani katika muziki wako.

“Mashabiki wana vitu vyao ambavyo wanataka kuvisikia au kuviona kutoka kwa msanii, unaweza ukawa na hit song kibao lakini ukashindwa kuzitumia. Kwa hiyo mimi binafsi tayari nimeshajua mashabiki wangu kwenye show huwa wanataka nini, ndo maana kila show ninayofanya lazima nifanye poa kwa sababu tayari nimeshajua nini wanataka mashabiki wangu,” alisema Bella.

Pia muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Nishike’ amewataka wasanii kuimba live na kwa hisia ili kuteka vizuri hisia za mashabiki wao.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment