TANZANIA: Sallam SK aeleza sababu za kufanya kazi na AY
16 March 2016

Baada ya msoto na hatimaye kufanikiwa kimuziki Ambwene Yesaya AY ametangaza rasmi kumpata mtu atakayesimamia kazi zake (Meneja) ambaye ni Sallam SK meneja mahiri kabisa wa masuala ya nje wa msanii nyota Diamond Plutnumz.

Ay, Sallam Sk pamoja na Hermy B
Meneja huyo wa Diamond Salaam SK katika mahojiano yake na kituo cha East Africa Radio amesema licha ya Ay kuwa na Connections za kutosha pamoja kujisimamia mwenyewe mda mrefu,ameamua kufanya naye kazi kwasababu ya uwezo mkubwa alionao wa kushawishi kufanya kazi na watu mbalimbali.Salaam sk and diamondSalaam amesema kuwa na connection ni jambo moja na kuweza kuzishawishi connections hizo ni jambo la pili, ingawa haimaanishi AY hawezi lakini amemuamini yeye kwajinsi alivyoona ushawishi wake.

AY
Pia Salaam ameongeza kuwa katika menejiment yake hafanyi kazi na mtu ambaye hajitumii katika kazi zake na kuongeza kuwa msanii lazima awe na ushawishi kwa meneja wake na kumlazimisha kufanya vitu ambavyo meneja akiona hawezi kuamini kama vingefanikiwa, akiwa na maana ya wivu wa maendeleo.
Chanzo: Mtembezi.com




Leave your comment