TANZANIA: Mchango wa muziki kwenye maisha ya Dayna Nyange.
15 March 2016

Hit maker wa Nivute kwako na sasa Angejua anae uwakilisha vyema mkoawa Morogoro maarufu kama Dayna Nyange amesema Mziki umemfanya kuheshimika katika jamii na kuondokana na utegemezi aliokuwa nao kwa ndugu.
Katika mahojiano yake na East Africa Radio Dayna amesema mwanzo alikua akitegemea mahitaji muhimu kutoka kwa ndugu zake lakini siku hizi anaweza kujitegemea kwa 100% na yote hiyo ni kwasababu ya muziki anaoufanya.Akielezea zaidi amesema yeye kama mwanamke hiyo imempa heshima pia kwa jamii kuwa ameweza kusimama peke yake bila kumtegemea mtu yeyote.




Leave your comment