Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: “Kwanini nifanye video Afrika Kusini?” – 20%
15 March 2016

Msanii Wa Muziki wa Bongo Fleva, Abbasi Hamisi ‘20 Percent’, amesema hatofanya video nchini Afrika Kusini kama wafanyavyo wasanii wengine kwa kuwa kwa sasa video zake ni za uswahilini hazihitaji kufanyika nchini humo.
Msanii huyo aliyewahi kunyakua tuzo 5 za Kili alisema licha ya kuwa na uwezo wa kufanya video za nyimbo zake nchini humo, lakini kwa sasa bado hana wimbo unaohitaji video kutoka huko. “Kwa sasa nina wimbo unaitwa ‘Mbaya hana Sababu’ ambao nitaufanyia hapa nchini na naamini video yake itakuwa bora na itafanya vizuri hata kama sitairekodia Afrika Kusini kama wafanyavyo wengine,” alisema 20 Percent.
Mkali huyo mwenye nyimbo za hisia aliongeza kwamba muziki wake si wa kushindana na msanii mwingine yeyote ndio maana hana haraka katika utoaji wa nyimbo zake pamoja na muziki wake. “Mimi sishindani na mtu katika muziki wangu nafanya kama akili yangu inavyotaka na nyimbo zangu natoa ninapoona nipo tayari kutoa na si kushinikizwa na watu,” alieleza.
Chanzo: Msetoea.com
Weekly Top 10 songs

Black Mark utandilubi omwami wangu5:21
KAPEKE LONDON2:23
In My Bed2:50
Paver2:55
CHAMPION GAL3:00
Ex Nkubilako ft DonMusa2:55
BIkola2:58
The Prelude of Grace1:31
Joy Is Coming3:08
Worship My King5:00
Top stories
- Excellent Jesus
26 May
- Trending song
24 May
- ICE PRINCESS SONGS
24 May


Leave your comment