TANZANIA: Post inayohisiwa ya Belle9 imemdis Diamond!!
3 March 2016

Hapo jana kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, msanii Belle9 alimake headlines kwa kuonekana post aliyoituma kwenyev account yake ikimdis Diamond Platnumz na kusema, “ kWa kuimba nenda kasome sio unitumie sms zako za ki***** me**** we kama utajili ni wako si hautuhusu **** acha kunizoea kijinga”. Baada ya muda stori zilianza kuzagaa mitandaoni kuwa post hiyo sio ya kweli huku wengine wakisema kuwa ni Belle 9 ndio kaandika post hiyo na kuifuta, baada ya hapo akatofautisha jina lake la instagrama kwa nukta ili hasijulikane kuwa kapost yeye.

Account ya Bellle 9 awali ilidaiwa jina kusomeka hivi, ila baada ya kupost picha na ujumbe huo na kufuta, account hiyo inatajwa kufanyiwa mabadiliko na kuondolewa nukta.
Leo asubuhi msanii Belle9 alipost na kuomba radhi kwa kitendo kilichojitokeza jana, na aliomba radhi kwa msanii mwenzake Diamond Platnumz, na kukiri kwamba si yeye aliyefanya kitendo hicho bali kuna hacker ambaye alikua anapost kutukana watu.






Leave your comment