TANZANIA: Amsha festival ndani ya Temeke.

 

Jumamosi hii katika viwanja vya Mwenye Yanga wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, kutakuwa na wasanii lukuki katika tamasha la Amsha Mama Festival 2016. Tamasha hilo ni hususani kwa kuhamasisha wanawake kujikwamua katika shughuli zao mbalimbali za kujikwamua kiuchumi. 

Khalid Ramadhani msanii wa muziki wa kizazi kipya alimaarufu kama ‘Tundaman’ ambaye pia ni balozi wa tamasha hilo amesema kuwa, “Tunapenda kuwaalika Watanzania wote kwa ujumla siku ya jumamosi hii ya Machi 5, mwaka huu waje kwa wingi katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar  Salaam, ili tujumuike kwa pamoja katika tamasha la kuhamasisha wanawake kujikwamua katika shughuli zao mbalimbali za kiuchumi” alisema Tundaman.

 

 

Balozi wa Amsha Mama Festival, Khalid Ramadhan 'Tundaman'

 

Aliendelea na kusema, ”Tamasha hili litakuwa ni la wazi kwa maana kwamba watu wote watapata burudani kibao bila malipo yaani bure kabisa hivyo waje kuwashuhudia wasanii kama, Khadija Kopa, Mr Blue, Snura, Msaga Sumu, Ali Chocky na Tunda Man wakitoa burudani ya hali ya juu kwani  ulinzi na usalama siku hiyo ni wa uhakika,” alisema Tunda Man.

Mratibu mkuu wa tamasha hilo Joe Kariuki  aliongezea na kuwataka wanawake hasa wanaojishughulisha na biashara za vitu mbalimbali kama mama ntilie, wauzaji wa mitumba na wauza matunda wahudhurie kwa wingi ili kuweza kupata fursa ya kunadi bidhaa zao na kutangaza bidhaa zao bure.

Leave your comment