TANZANIA: "Sifikirii kuoa for this time": Nay wa Mitego

 

Msanii wa miondoko ya hip hop Nay wa Mitego ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha shika adabu yako ambayo ilimpelekea kua gumzo ndani ya tasnia hii ya muziki, amesikika katika kituo cha East Africa Radio Jumatatu hii akisema kuwa hafikirii na wala hana mpango wa kuoa kwa sasa na wala hana mahusiano yoyote kwa sasa. Hivyo hawezi kukurupuka na kuchukua uamuzi wa kuoa.

"Kusema ukweli kabisa sijawahi kuulizwa swali ambalo sijaulizwa kwa muda mrefu, na nikiulizwa huwa nalikwepaga kufuatana na mahusiano ambayo nimekuwa nayo hapa katikati. Nashukuru Mungu amenijalia watoto so for this time nikianza kuongelea kuhusu kuoa nitakua najidanganya. Me sifikirii kuoa kabisa for this thime, kwa bahati mbaya au nzuri me sipo kwenye mahusiano na wala sitaki kukurupuka. Unajua ukifunga ndoa kwa sisi wakristo ndo nitolee. Yaani hapo umejicommit, umeshaingia kwenye 18 ambazo huwezi kupangua tena. Sifikirii kuoa, siwazi na sina mpango wa kuoa," alisema Nay.

Leave your comment