TANZANIA: Mr Nice aghairi kuachia video yake mpya kwa madai ya kuwa chini ya kiwango

 

Msanii mkongwe nchini, Mr Nice amesema ameshindwa kuachia video yake mpya ya ‘Kioo’ kwasababu ya kuwa chini ya kiwango, hivyo hali hiyo ingemshushia heshima.

Msanii huyo ameiambia tovuti ya Bongo 5 kuwa, tayari ameshashoot kazi mpya ambayo itatoka ikishakamilika.

“Video ya kioo tayari sema tumeshindwa kuitoa mimi na management yangu kutokana na kuwa chini ya kiwango. Kwahiyo tukashauriana na watu wangu tukaona hii sio kazi ya kwenda kwa jamii. Hivi sasa tayari tumeshoot nyingine kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula”, alisema Mr Nice.

Pia aliongeza kuwa hayupo kwa ajili ya kushindana na wasanii wengine kwani tayari alishafanya vitu vikubwa kwa wakati wake.

Leave your comment