TANZANIA: Lamar apata negative response toka kwa Producer wa Marekani..Fahamu ni kwanini!

 

Producer Lamar apata negative comment toka kwa Producer Scott Storch baada ya kupost video akiwa studio kwake na spika zikitoa mdundo mkali na kuandika caption yenye swali, “Ni msanii gani angefaa kupita juu ya huo mdundo” na kisha kumtag producer huyo.

Lamar kupitia caption yake alionyesha kuwa anajifunza vitu vingi kutoka kwake na kuwa inspired kupitia kazi za Producer huyo. Scott Storch ni producer mkubwa Marekani ambaye amehusika kutengeneza beat nyingi ikiwemo Naughty girl ya Beyonce, Sorry ya Rick Ross ft Chriss Brown pamoja na Make it Rain ya Fat Joe.

Kanye West akiwa na Producer Scott.

Comment zilisomeka hivi; ‘Kwanini unaweka beat zange kwenye Instagram yako? Lamar akajibu ‘Karibu kwenye ulimwengu wako boss, mimi shabiki wako mkubwa endelea kutuinspire’ Scott alimjibu .. ‘Tafadhali naomba usipost beat zangu ukajidai ni wewe umezitengeneza’.

Kisha Lamar akamjibu ‘Hakuna matata boss, haitatokea tena’ na kisha watanzania wengine wakaanza kucomment akiwemo Dogo Janja na Producer Lucci.

Pia baada ya tukio hilo, Lamar aliongea na Millardayo.com na kusema baada ya comment zile ilibidi amuandikie Scott message za private na kumwambia hakuwa na nia mbaya kwa alichokifanya, Scott alimjibu na kuwa mpole na kuelewa nia ya Lamar, akamjibu ‘Sawa kaka’.

 

Leave your comment