TANZANIA: Soma hapa alichokijibu Hascana baada ya Q Chief kudai directors wa ndani hawana lolote.
24 February 2016

Mmoja kati ya waongozaji video nchini, Hascana amjibu Q Chief kuhusu tuhuma alizotoa kwa directors wa bongo kuwa hawana lolote na hawezi kufanya nao kazi tena.
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumanne hii, Hanscana amesema Q Chief ana stress za maisha ndio maana amekuwa akiongea maneno ya ovyo.
“Ye ana stress za maisha, haiwezakani ukafanya muziki zaidi ya miaka 17 alafu huna hata pikipiki wakati kuna watoto wamekuja tu juzi kirahisi rahisi alafu wana kila kitu”, alisema Hanscana.
“Kwahiyo lazima upate mastress uanze kutapatapa, si unajua mfa maji, u can see yourself jamaa ana more than 17 years alafu he got nothing, alafu kuna watoto tu wadogo wanafanya kitu, kwahiyo unaweza ukafikiria suala dogo kama hilo kitaalamu hizo ni stress za maisha”, aliongeza Hanscana.
Muongozaji huyo wa video pia amemtaka Q Chief akae pembeni na kuwaachia wasanii wachanga wafanye kazi kwa sasa, nay eye abaki kuwa mtazamaji.
“Ninachomshauri atuachie tu new generation tufanye vitu vyetu, tuna mwaka mmoja kwenye game tuna drive, tunaishi vizuri, atuache tu vijana aangalie tu game awe anatuangalia YouTube”, aliongeza Hascana.




Leave your comment