TANZANIA: Video ya ‘Zigo Remix’ ya AY ft Diamond yafungiwa na TCRA

 

 

Rapper Ambwene Yesaya aka AY amethibitisha kupokea taarifa ya kufungiwa kwa video ya wimbo “Zigo Remix’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz.

Akizungumza na 255 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, Jumatatu hii, AY amesema alipokea barua yenye amri hiyo kutoka kwa rafiki yake ambaye anafanya kazi katika chombo kimoja cha habari.

“Sijaelewa ni maadili gani kwasababu kama maadili niliyokosea mimi ni kushoot kwenye swimming pool, na kama kwenye swimming pool watu nimevalisha jeans au maturubai hapo nitakuwa nimekosea maadili”, alisema AY.

“Mavazi ya kwenye swimming pool yako kila mahali, hata kwenye taarifa za habari (Michezo) wanaonyesha waogeleaji, kama hiyo pia ni kukiuka maadili ni sawa. Inashangaza mamlaka zetu inafocus kwenye kufungia nyimbo zetu na kuacha video za nje. Sijawahi sikia muziki wa Kenya, Uganda au Marekani umefungiwa, kama wanaona nyimbo za kina Nicki Minaj zina maadili halafu Zigo ya AY haina maadili baasi unaacha tu iwe ivyo”, aliongezea AY.

AY alisema barua hiyo ilitoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ikisema video hiyo inakiuka maadili.

Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi, amethibitisha kuvitumia vituo vya vya luninga nchini taarifa ya namna ya kupembua kazi za wasanii zisizo na maadili.

  

Leave your comment