TANZANIA: Madee atoa maamuzi ya Tip Top kuhusu Dogo Janja!
22 February 2016

Baada ya kuvuja sauti ya Dogo Janja akilalamika kuhusu uongozi wake wa Tip Top Connection kumbania. Madee ametoa uamuzi walioamua kuchukua.
Madee alisema kuwa hakuwa na taarifa yeyote juu ya malalamiko ya Dogo Janja ya kubaniwa hadi alipokutana nayo kwenye audio iliyosambaa mitandaoni, na kuongeza kuwa siku moja kabla ya audio hiyo kuvuja alikuwa na Dogo Janja wakimalizia video ya wimbo wake mpya na hakujua kama kuna tatizo lolote.
Madee ameyasema haya kama maamuzi ya Tip Top juu ya Dogo Janja;
“Mimi nabaki kwenye maamuzi ambayo tumeshaongea na Tale, kwamba hatuwezi kutoa maamuzi ambayo wao wanadhania yatakuwa ya kumkandamiza moja kwa moja Dogo Janja, kwasababu sawa mwanaume kama mwanaume anapoamua kutongoza unatumia mbinu zako nyingine tu, yeye ile ndio mbinu aliiona anaweza”, alisema Madee.
“Lakini kama kazi zake sisi tumeshazifanya na tumeshafanya kila kitu video tayari kwahiyo sidhani kama yale maneno yametoka moja kwa moja kwenye mdomo wake kina Madee wananibania wakati tayari kazi zake zimeshafanywa na ratiba yake imeshafanywa, nachoamini mimi ni kwamba alikuwa anataka tu kumuwin yule mwanamke, lakini kikubwa ambacho amehaaribu ni matusi pamoja na kutoa siri ambazo yeye anaona ni sawa kuzisema”, alieleza Madee.
Licha ya Dogo Janja kufanya hayo, Madee amesema kuwa hawatasitisha kutoa kazi zake ambazo zilikuwa kwenye ratiba kutoka.
“Ratiba lazima ziendelee kutoka kwasababu tayari tumeshapata hasara tumeshatoa hela za kufanya audio, video ratiba itaendelea lakini lazima Dogo Janja atakuwa chini ya adhabu”, alisema Madee.
Source: Millardayo.com




Leave your comment