TANZANIA: Afande Sele asema nyimbo za mabishano sio dili, awataka wasanii wa hip hop kuimba nyimbo za kujenga jamii!
19 February 2016

Msanii wa hip hop kutoka Morogoro, Afande Sele amesema wasanii kujibizana kwenye nyimbo kwenye nyimbo sio jambo la msingi kwani wanatakiwa waandae kazi ambazo zitajenga jamii na kuleta tija kwa taifa.
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Alhamisi hii, Afande alizungumzia wimbo wa Nay ‘Shika Adabu Yako’ na kutoa maoni yake juu ya wimbo huo kutokana na kuzungumzia watu mbalimbali.
“Nay kaimba kitu anachokiamini yeye na anachokiona yeye na ile ndio style yake ya muziki na hivyo inapotokea wewe unaanza kujibizana nae unakuwa ni wivu tu husda kwasababu yale ni mawazo yake yeye na ile ndio style yake na muziki wake ambayo imemtoa toka ameanza game, mimi nawashauri kuwa hawana sababu ya kujibu kwa vile nyimbo yenyewe tayari imeshafungiwa na imeonekana ina mapungufu mengi, mimi nadhani waache kama ilivyo waje na style nyingine muziki undelee mbele”, alisema Afande Sele.
Aidha Afande Sele amewataka wasanii kuacha kuimba nyimbo za kubishana kwani kuna vitu vingi vya kuimba ambavyo vitaleta tija kwa Watanzania.
“Ningependa kuwashauri wasanii kipindi hiki waimbe vitu vingi vya msingi ili wamsaidie Rais Mgufuli kuongoza nchi na mambo ya kujibizana wamuachie Isha Mashauzi na Khadija Kopa kwani ndio kazi zao”, aliongeza Afande Sele.




Leave your comment