TANZANIA: Tattoo, hereni na kufuga rasta ni mwiko mwilini mwangu – Ben Pol

 

Mwimbaji wa R&B,Benard Paul aka Ben Pol amesema kuwa hapendi kuchora tattoo, kuvaa hereni pamoja na kufuga rasta kama baadhi ya wasanii wengine wanavyofanya, kwakuwa anauheshimu sana mwili wake.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania, Ben Pol alisema kuwa imekuwa kawaida kwa idadi kubwa ya wasanii  kujichira tattoo na kuwa na mwonekano wa tofauti na watu wengine, lakini kwake suala hilo halina nafasi.

“Japo ni msanii lakini sipendi kuwa na mwonekano tofauti kama kufuga rasta, kuvaa hereni au kujichora mwilini kwasababu nauheshimu mwili wangu, ndio maana nipo kawaida kila wakati”, alisema Ben Pol.

Msanii huyo hivi karibuni ameachia wimbo uitwao ‘Nakuchana’ akiwa na Jux.

Leave your comment