TANZANIA: Kabla ya kuchana Young Killer alishawahi kuimba, soma zaidi hapa!
12 February 2016

Rapa Young Killer, amedai yakuwa kabla ya kuwa rapa amewahi kuimba kawaida.
Young Killer amesema kuwa amewahi kupata nafasi ya kurekodi kwa mara ya kwanza baada ya kusikia sauti yake inafananishwa na msanii wa Bongo Fleva Keisha.
Ameyasema hayo kwenye mahojiano na kituo cha Radio City FM wakati akiwa anatambulisha wimbo wake mpya uitwao ‘Insta Message’.
“Mimi nilikuwa mwimbaji, nimeimba sana …kwa Mfano Ali Kiba nimeimba album yake ya Cinderella yote”, alisema Young Killer.
“Nakumbuka kuna producer alikuwa ananifurahia kwasababu nilikuwa kachalii halafu kasauti kadogo, kanatoka kama Keisha anavyoimba ..basi jamaa akaniambia dogo nakupa ofa njoo urekodi’.
Msanii huyo mwenyeji wa jijini Mwanza ameachia wimbo wake mpya wa ‘Insta Message’.




Leave your comment