TANZANIA: Mysterio asema Riyama Ally ni Wife Material

 

Mwanamuziki Leo Mysterio ambaye ni mchumba wa nyota wa filamu nchini Riyama Ally, amesema Riyama ni mwanamke mwenye sifa ambazo alikuwa anazitafuta.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo Jumatano hii, Mysterio alisema muda wowote kuanzia sasa wanaweza kufunga ndoa kwani hatua za awali tayari wameanza kuzifanya.

“Unapopata mtu anayestahili kuwa mke usicheleweshe maamuzi ya kumuweka ndani”, alisema.

Pia aliongeza, “Unajua Riyama ni mtu ambaye ana huruma sana, ana akili pia ana mapenzi ya kweli kwangu amekuwa akinisaidia katika kazi zangu hivyo nimefikia wakati nimeona ni bora nimuweke ndani kwani nimeridhika na yeye kwa kila kitu, ndiyo maana sijataka kuchelewesha kwasababu yeye ndiye mwenye sifa kwangu”.

Licha ya hayo, Mysterio amesema hajakurupuka katika maamuzi alishafahamiana na Riyama kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita.

Leave your comment