TANZANIA: Kutoalikwa kwenye arobaini ya Tiffah, kwamliza baba yake Diamond!
8 February 2016

Baba wa nyota wa muziki Diamond Platnumz, Abdul Juma amesema hakuna siku alilia kwa uchungu kama siku ambayo mjukuu wake Tiffah alifanyiwa sherehe ya arobaini bila ya yeye kualikwa.

Akizungumza katika kipindi cha The Weekend Show cha Clouds TV jumamosi hii, Mzee Abdul alidai licha ya kuwa anawasiliana mara kwa mara na mama yake Diamond, lakini hakuwahi kupewa taarifa zozote kuhusu tukio hilo hadi alivyoona picha kwenye magazeti.

“Hakuna kitu kiliniuma kama kufanyiwa shughuli kwa yule dogo bila kualikwa”, alisema Mzee Abdul.

“Yaani nakumbuka nilipigiwa simu kuambiwa baba mwanao amepata mtoto lakini sio siku ya arobaini, niliumia sana, nililia, nililia sana kutoalikwa kwenye arobaini. Mimi nachoomba (Mama Diamond) asinisahau, kuna kazi nilifanya mpaka akawa hapo”, aliongeza.

Pia Mzee Abdula amemtaka mwane Diamond, afanye kazi kwa bidii.

“Mimi nampenda sana, kama kuna baya niliwatendea wanisamehe, mzazi hakosei, pia aendelee kujituma zaidi”, aliongeza Mzee huyo.

Leave your comment