TANZANIA: Masanja kufungua kituo chake cha Radio na Tv

Mchekeshaji maarufu wa kundi la Orijino Komedi, Masanja Mkandamizaji aweka wazi mpango wake wa kufungua kituo  cha Radio na Televisheni ambavyo atavisimamia yeye mwenyewe.

Akizungumza kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM Alhamisi hii, Masanja alisema tayari ameshapata mafunzo ya uandishi wa habari ili kujifunza kuhusu kuendesha vituo hivyo.

“Yea nimepanga kufungua kitu changu cha radio na Tv”, alisema Masanja.

“Nilikuwa na mpango wa muda mrefu ndio maana nikaenda shule ili kujifunza mambo mbalimbali kuhusu uendeshaji. Sasa hivi niko poa kabisa, najua vitu vingi hata nikiwaajiri watu hawata nidanganya kwasababu najua kila kitu”.

Licha ya kuwa ni muigizaji na mafanyabiashara, pia ni mkulima mkubwa wa zao la mpunga.

Leave your comment