TANZANIA: Adam Juma wa Visual Lab atoa somo kwa wanaoshoot video zao nje

Muongozaji wa video wa muda mrefu nchini, Adam Juma ameeleza madhara yanayotokea baada ya wasanii wa ndani kwenda kushoot video zao nje ya nchi na kutumia director wan je.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Adam ameandika;

“Katika hizi siku za karibuni kumekua na maswali mengi kuhusu wasanii kufanya kazi nje ya nchi, kila napopita swali ni hilo. Je kufanya kazi njee ya nchi ni sawa au si sawa? Jibu lake si rahisi na kiukweli linahitaji fikra kwa anayelijibu kulingana na nafasi yake. Industry ya  muziki ni pan asana, katika upana wake imewapa fursa vijana wengi, kwa mfano dancer na mavazi nk. Jambo hili kama nilivyosema awali usipo litafakari unaweza ukajibu kikawaida tu, ili industry ikue ushirikiano huu wa fani tofauti tofauti unahitajika sana. Nakumbuka shows zamani zilikata zikaja dar live mwaka mzima,ghafla ikawa bills na maisha, mpk sasa jiiii hamna kitu. Mdomo ukizoea mnofu mwishowe meno hugeuka kitoweo, show sikuhizi za kutafuta na haya yote ni madhara ya pupa.Wasanii wanaofanya video nje naamini wengi wanasababu za msingi bila fikra hawajui kinachotokea nyumbani, leo hii hakuna sababu mtu awekeze kwenye vifaa vya music video crew zinavunjika kila siku, models imekua story ndefu na mengine mengi yanajitokeza kila siku. Kinachosikitisha nipale unaposhoot video ya $10000 alafu ukirudi nyumbani unalia na mil 3 alafu watu wakiingia youtube director unanyewa kama mtoto wa kambo huku wakikulinganisha na director flani. Kweli kuna vitu wametuzidi lakini ubunifu nasie km watanzania tupo, tusitengeneze mazingira siku moja tuje kushindwa kufanya kazi hapa nyumbani. Kuna faida nyingi za kushoot njee tusijisahau, wanaija wameshtuka GOD anajua. Regards to all”.

Leave your comment