TANZANIA: Diamond yupo ‘Booked’ hadi May – Sallam
2 February 2016

Mmoja kati ya mameneja wanaomsimamia msanii Diamond, Sallam amesema kuwa msanii huyo tayari yupo booked kuanzia Februari hadi mwezi May.
Akizungumza na Swahili Radio Talk ya nchini Denmark, Sallam alisema yeye na mameneja wenzake wamehakikisha msanii wao anapata show za kutosha.
“Kila mwaka unapoanza ni lazima tuwe na ajenda ya kutengeneza program ya mwaka mzima, ndio maana mpaka sasa unakuta show zinaanza februari na tupo booked mpaka mwezi May” alisema Sallam.
“Kama mimi sahivi nipo Ulaya nafanya maandalizi ya tour yetu ya Ulaya na mambo yanaenda poa. Kwasababu watu wengi walikuwa wana hofu asije akatangazwa anakuja halafu asije ndio maana na mimi nipo huku kuweka mambo sawa” aliongeza.




Leave your comment