TANZANIA: Ray C asema haya baada ya tuhuma za kuhusishwa tena na ‘Matumizi ya madawa’

 

Msanii wa Bongo Fleva ameoneshwa kukasirishwa na taarifa zilizoandikwa kwenye magazeti ya Bongo ya Februari 1 na kukanusha tuhuma hizo.

Hivi karibuni magazeti yamekuwa yakiripoti kuwa muimbaji huyo amekuwa akionekana kwenye machimbo ya uuzaji wa dawa hizo jijini Dar es salaam.

Ray C pia amesema kutokana na taarifa hizo atakutana na watu hao mahakamani kwa taarifa hizo za uongo.

Hichi ndicho alichokiandika Ray C kupitia ukurasa wake wa Instagram;

“Seriously kwa kweli huwa naumia sana sana kuona binadam mwezangu anadiriki kuniharibia jina langu ilj yeye apate kula!hamjui mnaniathiri kiasi gani na hizi habari zenu?Hivi unadirikije kuandika usengwile kama huu bila hata aibu wala picha ya kuisapoti hiyo habari yani ni ujinga ujinga tu umeunganishwa na picha yangu bila hata uoga mmeichukua kutoka kwwnye page yangu ya insta bassss tayari mmeshapata story ili mradi tu mniharibie maisha yangu ili nyie mpate pesa mi nife maskini!!!

Kama kweli mnauhakika na mlichoandika kwanini hamkuweka picha yangu nikivuta hayo maunga badala yake mnaweka picha ya kituo cha mkunguni ambapo madaladala husimamisha kituoni hapo. Mmepiga picha ya kituo cha mkunguni mkaona haitoshi mkaingia kwenye page yangu ya insta na kuchukua picha yangu niliojipiga mwenyewe ndio mnazitumia kunichafulia jina langu tena wakati ndio kwanza nahangaika kurudi tena kwenye kazi yangu.”

Haki ya mungu sijawahi kuskia hata siku moja nyie mmeandika kuhuau foundation yangu na mambo mazuri iliofanya,je mnajua kama mpaka sasa nimeshatoa vijana zaid ya sabini kwenye madawa na wako fit wanatumia methadone je mnajua hilo?Hata siju moja sikawahi pata msaada wowote kutoka kwenu japo kunichangia nauli. Tu ya kuja kwenye dawa kila siku hakuna hata anaenisaidia huu mwaka wa tatu bado naendelea kunywa dawa na ni kila siku ya mungu siku saba kwa wiki hakuna sikukuu wala msiba na ukikosa mwili unauma vibaya sana yani its not easy but am a [expletive] hard working woman na ni mwanamke jasiri napambana na siogopi kujaribu,naparangana na haya madawa na nayapinga na kamwe sintorudi nyuma na hizi nuksi mzipeleke kwenye familia zenu,wewe shigongo unamkosea sana mungu!unajifanya mlokolw lakini kazi yako ni kuharibia maisha ya wenzio unasahau kuwa malipo ni hapahapa duniani!Mimi ni kapuku tu sina mbele wala nyuma mbele yako lakini bado unanichimbia kaburi angali mi mzim

Na wewe Mayasa Marwata ni [abusive text] usie jua kazi yako!nimeisoma stori yako nimegundua ni mvivu wa kufatilia habari!Eti Chimbo LA unga langu lajulikana sasa kama ushalijua mbona haukunipiga nikivuta huo unga unaenda kupiga picha kituo cha daladala bwege we! Ntapambana na nyie MAHAKAMANI. (sic)” 

 

Leave your comment