TANZANIA: Diamond adai anamuona Zari bado mbichi kama embe la msimu!

Ikiwa bado kuna watu wanaodhani kwa kuwa ni mama wa watoto 4, Zari anaweza kuwa ameshapoteza sifa za ‘usichana’, lakini hiyo ni tofauti na Diamond.

Hitmaker huyo wa ‘Utanipenda’ anamuona Zarithebosslady kama msichana mbichi na hauchoki uzuri wake.

“I swear I can’t get used to your Cuteness…Kadada Kabiichi…Kama Embe la msimu” aliandika Diamond wenye picha ya mama wa mtoto wake Tiffah.

Zari yupo Dar es salaam kwa siku kadhaa na ametumia fursa hiyo kumsaidia mzazi mwenzie kupanga mikakati mipya ya WCB.

“Calling shots …late night strategic planning. All we see is dollar signs at WCB Empire” aliandika Zari.

 

Leave your comment