EXCLUSIVE (TANZANIA) – Wasanii tusifanye vitu kwa kukariri – Joh Makini
22 January 2016

Rapa wa kundi la Weusi, Joh Makini amesema wasanii wasijifunge kwa kuachia nyimbo chache kwa mwaka na kusubiri nyimbo ichuje ndio waingie studio kurekodi wimbo mpya.

Msanii huyo amesema hayo wakati akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM jumamosi iliyopita, Joh alisema redio nazo ziwe tayari kupokea muziki mzuri bila kujali msanii anatoa nyimbo ngapi kwa mwaka.

Aliongeza kuwa wasanii wanapaswa kuwa wepesi kujifunza mambo mapya na kuacha kukariri mambo.

“Tumekariri kwamba siwezi kuingia studio wakati mwingine kutengeneza wimbo mpaka nitakapoona wimbo niliotoa ambao unafanya vizuri uanze kuchuja”, alisema Joh.

“Hiyo inasababisha muziki unaozalishwa unakuwa mdogo. Tujenge mazoea na media pia zifungue milango wazi bila kusema wewe una ngoma nyingi, una ngoma kali inayofanya vizuri sasa hivi usitoe nyingine”, aliongeza.

Amevitaka vituo vya redio kupokea muziki mzuri muda wowote na kutoka kwa wasanii wote.

Leave your comment