EXCLUSIVE (TANZANIA) – Sitaki kuwa karibu tena na Kajala – Wema

 

Wema Sepetu amesema hataki tena kuwa karibu na rafiki yake wa zamani Kajala Masanja kwa madai kuwa alishindwa kumtafuta na kumuomba msamaha kwa makosa aliyoyafanya.

Akiongea katika kipindi cha Take One cha Clouds TV, Wema alisema Kajala kwa sasa anamchukulia kama mtu asiyemfahamu.

“Mimi mtu ambaye sitaki nijiassociate naye namtoa kabisa ndio maana naweza nikakaa nikakuuliza Kajala ndio nani? Huu sio muda wa kumzungumzia na kumpa airtime”, alisema Wema.

“Kwasababu nilishasemaga hata kwenye kipindi changu najuta kumsaidia”.

Pia Wema aliongeza Kajala hajawahi kumuomba msamaha yeye mwenyewe tofauti na ile post ya Instagram aliyoomba radhi. Wema pia anadai ameshamu unfollow na kumblock Kajala kwenye Instagram.

Pichani Kajala Masanja.

 

“Mimi sina kinyongo na mtu, unajua mtu ambaye ana kinyongo na mtu ni mtu ambaye hawezi kukaa bila kumuongelea mtu fulani. Mimi sijawahi kukaa na kumuongelea Kajala na nimemchukulia kama ni mtu ambaye ameshapita kama upepo. Hajui kuutumia utu uzima wake ni mtu mzima for nothing, ni mtu mzima fulani lakini hana akili. Pia naona sio tu hana akili hata washauri wake ni wabaya”, alisisitiza Wema.

Pia Wema alifafanua kiini cha ugomvi wao na nani alisababisha.

“Kajala mimi ndiye alinizingua Mungu anajua kila kitu. Lakini mimi sikwenda kwenye Instagram kupost na kuandika Kajala kanizingua, mimi nilimfata Kajala personal kwenye meseji nikamfuata nikamwambia nilichoweza kumwambia na hakukiona kwenye Instagram hata kumwambia najuta kumsaidia nilimwambia kwenye kipindi lakini nilianza kumwambia kwenye meseji”.

Miaka miwili iliyopita, Wema alimlipia Kajala shilingi milioni 13 ili asifungwe jela kwa msala wa kutakatisha fedha aliokuwa unamkabili.

Mwaka 2015 wawili hao waliokuwa marafiki wakubwa waligombana kwa madai Kajala alitoka kimapenzi na mpenzi wa rafiki yake, Wema.

 

Leave your comment

Top stories