EXCLUSIVE (TANZANIA) – Video kali ni moja ya sababu inayosaidia wasanii kutoka kimataifa - Mr Blue
21 January 2016

Msanii Mr Blue asema kuna sababu kubwa tatu zilizosababisha wasanii wa muziki wa kipindi cha nyuma kushindwa kutoboa kimataifa.

Msanii huyo anayetamba na video aliyotoa hivi karibuni wa ‘Baki na Mimi’, amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM jumatano hii kuwa moja ya sababu ni wasanii kuona wao ni wa hapa hapa.

“Ni kama vitu vitu vitatu cha kwanza nina weza kusema wakati tunaanza muziki soko letu tulikuwa tunawaza hapa na hizo nchi zetu za karibu ambazo ni Kenya na Uganda”, alisema.

“Kwahiyo kilichotufanya kutokufika huko ni kutokujua hicho. Cha pili ni connection kwasababu watu unawaona wanachezwa kwenye hivyo vyombo vikubwa wengi sio kwamba wana video nzuri wengine ni connection na wale watu wa vituo”, aliongeza Blue.

“Na cha tatu ambacho kinasaidia kweli ambacho tulikuwa tunakidharau ni video kali. Kuwa na video kali nayo inasababisha watu wa kule pia kuipenda na kuona kweli hii inafaa kuchezwa kwenye kituo chetu”.

Hata hivyo mpaka sasa Mr Blue hajawahi kuwa na video iliyofanikiwa kimataifa kama za wasanii wengine wa hivi karibuni.

Leave your comment