EXCLUSIVE (TANZANIA) – Zari na Wema kurushiana maneno ya kashfa Instagram
19 January 2016

Kupitia ukurasa wa Instagram vita vikali vya kurushiana maneno ya kashfa kati ya Zarina Hassan (Zari The Boss Lady) na Wema Sepetu. Vita hivyo vilianza baada ya maneno kutoka kambi ya Wema kwenda kwa Mama Tiffah.
Ambapo mwisho wa siku Zari aliamua kutoa ya moyoni kwa kuweka comment chini ya picha yake mwenyewe baada ya matusi kutoka kambi ya Wema kuzidi.
“Fake cars, fake houses, fake men, fake everything but they are here to judge… ya’ll look like just had a fight with a tiger”, aliandika Zari.
“We feel your pain Dee is a loving man. I know what you missing but guess what I got it all by myself. Sent to hell on a one way ticket buried 6ft under #Kasepa #HeIsHappyNow”, aliongeza Zari.
Ambapo naye Wema hakukaa kimya na kujibu mashambulizi.
“Damn she really got da energy”, aliandika Wema.
“Mi siwezi jamani mambo haya. Kaka kajua kamchanganya dada. Sasa kama kachanganyikiwa si yeye. Mi ningejua kama kuna siku ningekuja kummiss kaka nisingemwacha. Akumbuke hilo kwanza.Halafu kingine mi ni mwanamke pekee niliyewahi kuwa na kaka au?
“Maana naona wenzangu hawatajwi ni Wemaa tu. Kuna kitu dada anakitafuta kwangu jamani. Sasa dada kama atasoma hapa ajue kuwa this is 2016, afanye mabadiliko basi tokea 2014 ana mimi tu, 2015 ana mimi tu na 2016 pia! Baby hujachoka tu? Nimejibu kwa mara ya kwanza maana naona umekuwa ukinitafuta muda mrefu mno. Mi maneno kama yako sijui fake sinaga.But just if you read this honey, pliz nitoe kwenye ramani yenu. I know longer live there. And kuhusu kuwa fake, mi nishajikubali na fake life yangu ila ningeomba utuwekee DNA ya Baby Tee kwanza. Pumbavu”.
Zari aliusoma ujumbe huo na kujibu;
“Ati DNA for what let her start na DNA ya Swiss then atupe Ultrasound kisha ampime mtoto wake then she can ask for Tiffah’s. Hujawahi kuingia labour ati unaomba DNA. Wacha na mambo ya wazazi. Endelea kugawa that’s the only thing you can manage. Mtoto wangu asikupe stress don’t beef with a baby, find your levels, Tiffah level nyingine #BabyBoss”.
Wema alijibu bila presha na kuandika post; “Mama taught me well …! Kugombana na mtu mzima ni kukosa adabu …Sijafunzwa Hivyo…!”.




Leave your comment