EXCLUSIVE (TANZANIA) – Babu Tale asema haya baada ya kauli ya Diamond kuhusu kupitisha video MTV Base

 

Wiki iliyopita story ya Diamond ilizagaa kuhusu kupitisha video MTV Base, baada ya kufanyiwa interview na TBC FM kwenye kipindi cha Papaso ambapo miongoni mwa maswali aliyoulizwa ni namna ipi anawasaidia wasanii wa Tanzania baada ya kusemekana yeye anawabania nje ya nchi.

Jibu alilotoa Diamond alisema kuwa huwa hawabanii Watanzania wenzake na ndiyo sababu hata video za wasanii wa Tanzania zinapofika MTV Base hupigiwa simu na kuulizwa, kauli hii imeleta utata hadi kufikia Uongozi wa Diamond umeamua kutolea ufafanuzi.

Babu Tale alihojiwa na XXL ya Cloud FM na kusema “Ingekuwa ni kweli wimbo wa Harmonize ambae ni msanii wa Diamond ungekuwa unapigwa kila siku au ungekuwa Exclusive MTV sababu ndio biashara yake, hilo sio neno la ukweli… yule aliyetoa habari amekichukua kichwa cha habari na kukifanya habari kwa watu wengine”.

“Diamond aliulizwa Wasanii gani ambao amewasaidia na anasupport muziki nyumbani kwenda nje, akajibu mimi mbona huwa nsaidia watu wengi? Na kuna kipindi mtu huwa ananipigia simu unamjua flani? Ni mzuri? Kuna media za nje huwa zinanipigia kuniuliza kama namjua flani? Hivyo tu nayeye huwa anasema ni mzuri ili Watanzania wapae”,alisema Babu Tale.

Pia Babu Tale alimaliza kwa kusema ‘Aliyeandika kichwa cha habari akasema DIAMOND NDIYE ANAAMUA MTU FLANI KUCHEZWA SEHEMU TV FLANI, sio kweli .. kama Diamond angekua anaamua hivyo basi nyimbo zote za TMK, Mkubwa na wanae na wote wa karibu na Diamond zingekuwa zinapigwa sana MTV’.

Leave your comment